SiasaTunisia
Upinzani wakosoa uchaguzi wa rais Tunisia
6 Oktoba 2024Matangazo
Uchaguzi huo unamkutanisha rais aliye madarakani Kais Saied na wapinzani wawili pekee ambao mmoja wao yuko jela.
Mapema wiki hii, mahakama ya Tunisia ilithibitisha kifungo cha miezi 20 kwa mgombea urais Ayachi Zammel, mfanyabiashara na mwanasiasa huria, kwa tuhuma za kughushi ridhaa ya uchaguzi.
Soma pia: Mgombea urais Tunisia ahukumiwa miaka 12 jela
Vyama vya upinzani na mashirika ya haki za binadamu yanasalia kuwa na mashaka kuhusu haki ya uchaguzi, huku Tume ya uchaguzi hivi majuzi ikikataa kuwaruhusu wagombea wengine watatu wa urais walioruhusiwa na mahakama kujumuishwa kwenye kinyangayiro hicho baada ya kukata rufaa.