1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya upinzani India vyasusia uzinduzi wa Mordi

28 Mei 2023

Vyama vikuu vya upinzani nchini India vimesusia ufunguzi wa majengo ya bunge uliofanywa na waziri mkuu Narendra Mordi, katika kitendo cha nadra cha mshikamano dhidi ya chama tawala cha Hindu Nationalist

https://p.dw.com/p/4Rv0F
Indien | Einweihung neues Parlamentsgebäude in Neu-Delhi
Picha: India's Press Information Bureau/REUTERS

Chama hicho tawala cha Mordi kimekuwa madarakani kwa miaka 9. Vyama hivyo vya upinzani vimekosoa tukio hilo mjini New Delhi vikidai kuwa Mordi amemtenga Rais wa India Droupadi Murmu ambaye ni mkuu wa nchi. Zaidi ya vyama 19 havikushiriki sherehe hizo zilizofanyika siku moja na maadhimisho ya kuanzishwa kwa itikadi ya chama tawala cha waziri mkuu Mordi.

Wakati wa uzinduzi huo, waziri mkuu huyo wa India alitoa hotuba ya dakika 40 ambapo alilipongeza bunge la India kwa kuwa na demokrasia. Aliongeza kuwa taifa hilo limeachana na enzi ya kikoloni akizungumzia jengo la awali la bunge lililojengwa wakati Uingereza ilipoitawala India.