Upinzani Zambia kumshtaki Lungu
23 Machi 2018Matangazo
Hoja hiyo ya chama cha United Party for National Development, UPND, ilisainiwa na theluthi moja ya wabunge wote katika bunge la Zambia lililo na viti 166, lakini itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge ili kupitishwa. Msemaji wa rais amesema hoja hiyo ni muendelezo wa kile alichokiita 'njama zilizoshindwa za chama cha UPND', kumuondoa madarakani rais Edgar Lungu, ambazo amesema hazitafika popote. Hoja ya chama cha UPND inasema Rais Edgar Lungu alikiuka katiba ya nchi, pale alipokaidi kuyakabidhi madaraka kwa Spika wa Bunge, baada ya upinzani kuanzisha kesi kortini kupinga ushindi wake.