1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi imezuia mashambulizi katika eneo la Donetsk

5 Juni 2023

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa vikosi vyake vimezuia mashambulizi makubwa katika eneo la kusini mwa Ukraine la Donetsk na kuua wanajeshi wapatao 250 wanaoungwa mkono na utawala wa Kyiv.

https://p.dw.com/p/4SCQJ
Ukraine Donezk Region | Gefangenenaustausch
Picha: Yevhenii Zavhorodnii/REUTERS

Taarifa ya wizara hiyo imebaini kuwa Ukraine ilianzisha mashambulizi makubwa siku ya Jumapili kwa kutumia vifaa kadhaa vya kivita. Hata hivyo, shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha mara moja taarifa hizo kutoka kwaUrusi.

Soma pia: Urusi yashambulia maeneo ya jimbo la Donetsk

Haikubainika pia kuwa shambulio hilo ndio mwanzo wa mashambulizi ya Ukraine ambayo yalikuwa yakitarajiwa kwa muda mrefu ili kuwania udhibiti wa baadhi ya maeneo yaliyonyakuliwa na vikosi vya Urusi mara tu baada ya uvamizi huo, Februari mwaka jana.

Mapema leo asubuhi, Gavana wa jimbo la Urusi laBelgorod Vyacheslav Gladkov amesema kuwa kituo cha nishati kimeshambuliwa na ndege zisizo na rubani na kwamba bado kunashuhudiwa moto mkubwa eneo hilo.