1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kuchukuwa nafasi ya Ukraine ngano ya Afrika - Putin

27 Julai 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameuambia mkutano wa kilele wa Urusi na viongozi wa Afrika mjini Saint Petersburg leo kwamba nchi yake inaweza kuchukua nafasi ya Ukraine katika kupeleka nafaka barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4USNu
Russland Moskau | Präsident Putin leitet Videokonferenz zu wirtschaftlichen Themen im Kreml
Picha: Alexander Kazakov/AP Photo/picture alliance

Putin ameongeza kwamba Urusi itakuwa tayari kusafirisha nafaka bila malipo kwa nchi sita za Afrika katika kipindi cha miezi mitatu au minne ijayo.

Kiongozi huyo wa Urusi alisema nchi hizo ni Burkina Faso, Zimbabwe, Mali, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Eritrea.

"Kila nchi itapata kati ya tani 25,000 na 50,000." Alisema akiongeza kuwa ananuwia kuendeleza juhudi za amani zilizoanzishwa na mataifa ya Afrika ili kuupatia ufumbuzi mzozo wa Urusi na Ukraine.

Soma zaidi: Urusi inataka nini Afrika?

Urusi yakataa kurefusha mkataba wa nafaka, dunia yalalamika

Kulingana na Kremlin, wawakilishi kutoka mataifa 49 kati ya 54 ya Afrika wanahudhuria mkutano huo wa kilele huku 17 kati yao wakiwa marais.

Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na mkutano wa kwanza mnamo mwaka 2019 huko Sochi.

Urusi imezituhumu nchi za Magharibi kwa kuziwekea shinikizo nchi za Afrika kutohudhuria mkutano huo.