SiasaUrusi
Urusi kujadili muswada juu ya wakosoaji wa jeshi lake
20 Januari 2024Matangazo
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, muswada huo ambao unaungwa mkono na wabunge wote nchini humo, utawasilishwa bungeni siku ya Jumatatu ili ujadiliwe.
Moscow imefanya ukosoaji wa jeshi kuwa kosa baada ya kuivamia Ukraine mnamo mwezi Februari 2022, na imewakatama maelfu ya watu wanaopinga uvamizi huo.
Vyacheslav Volodin amesema hatua hiyo inalenga kuwaadhibu wale aliowaita "mafisadi" ambao wanalipaka tope jeshi la Urusi na maafisa wengine wanaoendelea na oparesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.