SiasaUrusi
Urusi: Mafuta hayataathiri mashambulizi nchini Ukraine
5 Desemba 2022Matangazo
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi habari kwamba uchumi wa Urusi una uwezo kamili wa kumudu gharama na mahitaji yote ya operesheni zake katika vita vinanyoendelea nchini Ukraine.
Kwa mara nyingine Peskov amesisitiza pia kuwa Urusi haikubaliani na uamuzi huo wa kuwekwa ukomo wa bei kwa mafuta yake na ameapa kwamba Moscow itajibu hatua hiyo ya nchi magharibi.
Umoja wa Ulaya, kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi la G7 na Australia yalitangaza mwishoni mwa juma lililopita makubaliano ya kununua mafuta ya Urusi kwa bei isiyopindukia dola 60 kwa pipa, uamuzi unaolenga kuhujumu mapato ya Urusi kwenye sekta yake ya nishati.