Urusi: Mripuko katika daraja la Kerch ni tendo la ugaidi
17 Julai 2023Tukio hilo lililoelezwa hapo awali na viongozi wa eneo hilo kuwa la dharura, lilisababisha magari kusimamishwa kwenye kivuko hicho kinachotumika kwa shughuli nyingi.
Msemaji wa kamati ya uchunguzi ya Urusi, Svetlana Petrenko, amesema, kamati ya Uchunguzi ya Urusiilianzisha kesi ya jinaichini ya Kifungu cha 205 cha Kanuni ya Jinai ya Shirikisho la Urusi, yaani, kitendo cha kigaidi.
Soma pia:Urusi: Daraja muhimu la Krimea laharibiwa na mlipuko wa lori
Aliongeza kwamba kulingana na uchunguzi huo, usiku wa Julai 16-17, kama matokeo ya kitendo cha kigaidi kilichofanywa na huduma maalum za Ukraine, sehemu moja ya daraja hilo la Crimea iliharibika.
Spika wa bunge la Crimea, eneo lililotekwa na Urusi mnamo mwaka 2014, Vladimir Konstantinov, ameilaumu Ukrainekwa shambulio hilo jipya.