1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi na China zasaini mikataba ya kiuchumi

24 Mei 2023

Urusi na China zimesaini mikataba kadhaa ya kiuchumi, huku kukiwa na ukosoaji wa mataifa ya Magharibi kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4RleI
China Russland l Wirtschaftsforum in Shanghai l Premierminister Mikhail Mishustin
Picha: Dmitry Astakhov/dpa/picture-alliance

Ukosoaji dhidi ya hatua hiyo ni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili wakati vita vya Ukraine vikiendelea.

Waziri Mkuu wa Urusi, Mikhail Mishustin anaizuru China ambako amekutana na Rais Xi Jinping pamoja na Waziri Mkuu, Li Qiang.

Xi amemueleza Mishustin kwamba China na Urusi zitaendelea kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi ya kila mmoja na kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kimataifa.

Katika mkutano wake wa Li, Mishustin amesema kwamba uhusiano kati ya Urusi na China uko katika kiwango cha juu sana.

Mitakaba iliyosainiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji katika huduma za biashara, mauzo ya bidhaa za kilimo kwenda China, na ushirikiano wa michezo.

China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Urusi.