1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zote zimefanya uharibifu

6 Julai 2024

Mamlaka za Uruisi na Ukraine zimesema kwamba mataifa hayo mawili yamefanya uharibifu mkubwa katika nchi hizo mbili unaotokana na mashambulizi ya droni yanayoendelea baina yao

https://p.dw.com/p/4hy2N
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Picha: KIRILL CHUBOTIN/Ukrinform/IMAGO

Mamlaka za Uruisi na Ukraine zimesema kwamba mataifa hayo mawili yamefanya uharibifu mkubwa katika nchi hizo mbili unaotokana na mashambulizi ya droni yanayoendelea baina yao.

Jeshi la anga la Ukraine katika ripoti yake iliyotolewa hii leo limesema Urusi ilishambulia maeneo yake 12 huku droni 24 kati ya 32 zikidunguliwa. Mashambulizi hayo yalisababisha kukatika kwa umeme na maji katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Sumy. Katika mji wa Kiev makazi ya watu na magari yameharibiwa kufuatia shambulizi la droni la Urusi.

Soma zaidi.Waziri mkuu wa Hungary afanya ziara nchini Urusi

Kwa upande mwingine, katika miezi ya hivi karibuni, Ukraine nayo imekuwa ikiyalenga maeneo ya kijeshi na maeneo ya kuhifadhi mafuta ya Urusi na kupelekea changamoto ya usafirishaji kwa Urusi katika vita hivyo vilivyodumu zaidi ya miaka miwili sasa.