1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi: Ukraine yatumia makombora ya Uingereza kuwalenga raia

13 Mei 2023

Urusi imesema kuwa Ukraine imetumia makombora ya masafa marefu ya Uingereza kuyalenga maeneo ya kiraia katika mji wa mashariki wa Lugansk na kuwajeruhi watoto sita.

https://p.dw.com/p/4RJAI
Ukraine Krieg | Ukrainischer Angriff auf Luhansk
Picha: Vladimir Ivanov/TASS/IMAGO

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema Ijumaa usiku kuwa vikosi vya jeshi la Ukraine vilishambulia maeneo mawili ya raia

Kwa mujibu wa wizara hiyo, ndege ya kivita chapa Sukhoi Su-24 iliyokuwa imebeba makombora hayo, na ndege ya kivita chapa MiG-29 zimedunguliwa.

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Jumamosi aliwasili Roma na kupokelewa na Rais wa Italia Sergio Mattarella kwenye makaazi yake rasmi. 

Mattarella amekuwa akionyesha mshikamano na Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi. 

Zelensky ambaye anatarajia kuiomba Italia msada zaidi, atakutana pia na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Aidha, siku ya Jumapili Zelensky anatarajiwa kuwasili mjini Berlin, Ujerumani.