1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yadai kuzima mashambulizi mengine ya Ukraine

6 Juni 2023

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa imezima mashambulizi mengine makubwa ya vikosi vya Ukraine huko Donetsk, na kusababisha hasara kubwa kwa majeshi ya Kyiv na kuharibu vifaru vinane vya kivita chapa Leopard.

https://p.dw.com/p/4SEuC
Leopard 2 A6 Panzer
Kifaru chapa Leopard 2 A6 Panzer Picha: Christoph Hardt/Panama Pictures/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mapema leo kuwa imezima mashambulizi mengine makubwa ya vikosi vya Ukraine huko Donetsk, na kusababisha hasara kubwa kwa majeshi ya Kyiv na kuharibu vifaru vinane vya kivita chapa Leopard. Jana, Urusi ilisema kuwa Ukraine imeanzisha mashambulizi makubwa katika mkoa huo wa kusini. Maafisa wa Ukraine wamethibitisha kuanza mashambulizi makubwa katika baadhi ya maeneo na kusema kuna mafanikio yanayodhihirika huko Bakhmut. Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ganna Malyar amesema Urusi imekuwa ikitoa taarifa hizo mara kwa mara ili kuficha ukweli kwamba wamekuwa wakishindwa mapambano huko Bakhmut. Urusi na Ukraine zimekuwa zikidai kusababisha hasara kubwa kwa upande mwingine, taarifa ambazo mara kadhaa zimekua vigumu kuthibitishwa.