Urusi yaingia mkataba na Kazakhstan
21 Desemba 2007Matangazo
MOSCOW.Rais Vladmir Putin wa Urusi na Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan wametiliana saini makubaliano ya kujenga bomba kubwa la gesi kutoka Turkeministan kwenda Urusi kupitia Kazakhstan.
Mpango huo ni mikakati ya Urusi ya kusambaza nishati hiyo kwa nchi za Umoja wa Ulaya zinazoihitaji kwa kiasi kikubwa.
Urusi inahitaji kujenga bomba la gesi kutoka Asia ya kati ili kukidhi mahitaji ya wateja wake wa wa Ulaya.