Urusi yaionya Japan kuipa Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga
27 Desemba 2023Matangazo
Amesema hilo linatishia kuharibu uhusiano wa Japan na Urusi. Wiki iliyopita Japan ilisema inajiandaa kupeleka mifumo hiyo ya ulinzi wa anga nchini Marekani baada yakupitia kanuni za usafirishaji wa silaha zake.
Licha ya kanuni za taifa hilo la Asia kuizuwia nchi hiyo kusafirisha silaha kwa nchi zilizo vitani, inaweza kuifaidisha Ukraine sio moja kwa moja, kwa kuipa Marekani silaha ili Marekani izisafirishe mjini Kiev.
Soma pia:Ukraine yasema imedungua droni za Urusi
Mahusiano kati ya Moscow na Tokyo ambayo tayari yanayumba yamezidi kuingia doa tangu Urusi ilipotuma maelfu ya wanajeshi wake nchini Ukraine Februari mwaka 2022, baada ya hapo Japan ilijiunga na washirika wa Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi kufuatia hatua yake hiyo.