1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yamuonya balozi wa Marekani kuingilia mambo ya ndani

7 Machi 2024

Wizara ya masuala ya kigeni ya Urusi imemuita balozi wa Marekani mjini Moscow Lynne Tracy, kumuonya kwamba itawaondoa wanadiplomasia wote wa Marekani nchini humo iwapo taifa hilo halitoacha kuingilia mambo yake ya ndani.

https://p.dw.com/p/4dGhs
Balozi wa Marekani mjini Moscow Lynne Tracy
Urusi imemuonya balozi wa Marekani mjini Moscow Lynne Tracey (pichani) kwa kuingilia mambo yake ya ndaniPicha: Vladimir Astapkovich/SNA/IMAGO

Wizara ya masuala ya kigeni ya Urusi imesema imemuita balozi wa Marekani mjini Moscow, Lynne Tracy, kumuonya kwamba itawaondoa wanadiplomasia wote wa Marekani nchini humo iwapo taifa hilo halitoacha kuingilia mambo yake ya ndani.

Moscow imetoa onyo hilo kuelekea uchaguzi wake mkuu utakaoanza tarehe 15 hadi 17 Machi ambao Rais Vladimir Putin, ambaye tayari ameshaiongoza Urusi kwa miaka 20, ana uhakika wa kushinda tena.

Wizara hiyo kupitia taarifa yake imesema itaangalia kile ilichokiita "hatua za kichokozi" na kusambazwa kwa taarifa zinazohusiana na uchaguzi na operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

Imeongeza kuwa maafisa wa Marekani watakaopatikana na makosa hayo huenda wakafukuzwa kabisa nchini humo.

Hata hivyo, msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Moscow amesema hawana chochote cha kusema juu ya hili.