1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaongeza hujuma nchini Ukraine msimu huu wa baridi

8 Februari 2023

Wanajeshi wa Urusi wameimarisha mashambulizi, msimu huu wa baridi kali mashariki mwa Ukraine, huku wakiwaleta malefu ya wanajeshi wapya kwenye uwanja wa mapambano.

https://p.dw.com/p/4NDsP
Ukraine Donetsk Straße Munitionsteile
Picha: Nikolai Trishin/TASS/dpa/picture alliance

Ukraine inatarajia Moscow kutanua operesheni yake wakati miji ya kaskazini mashariki na kusini ikikumbwa na mashambulizi makali. Jeshi la Ukraine limesema askari 1,030 wa Urusi waliuawa katika kipindi cha masaa 24, ikiwa ndio idadi kubwa kabisa kutokea kwa siku moja katika vita hivyo.

Haijawezekana kuthibitisha kwa njia huru idadi hiyo ya vifo, na Urusi pia imedai kuwauwa wanajeshi wengi wa Ukraine katika wiki za karibuni. Urusi ilisema iliwauwa askari 6,500 wa Ukraine katika mwezi wa Januari.

Nchi tatu za Ulaya - Ujerumani, Uholanzi na Denmark zimetoa ahadi ya kuipatia Ukraine vifaru chapa Leopard 1 visivyopungua 100 katika muda wa miezi michache ijayo.

Haya yanajiri wakati waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius akifanya ziara ya kushtukiza nchini Ukraine, wiki mbili baada ya serikali mjini Berlin kutoa ridhaa ya kuipa Ukraine vifaru vya kisasa, kufuatia shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wake.