Urusi yataka UN kuingilia mazungumzo ya nafaka
20 Julai 2022Lavrov amesema Urusi ilikubali kile alichokiita "kanuni za kimsingi" kuhusu usafirishaji wa nafaka na Ukraine, lakini ujumbe wa Ukraine umekataa kujumuisha kifungu cha kulinda mauzo ya nje ya Urusi.
Ukraine na Urusi zimefanya mazungumzo chini ya upatanishi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa ili kuruhusu usafirishaji wa nafaka katika soko la kimataifa, wakati meli za kutoka bandari za Ukraine zikizuiwa kutokana na mashambulizi ya jeshi la Urusi.
Kauli ya Lavrov ameitoa siku moja tu baada ya rais Vladimir Putin kusema wakati wa ziara yake nchini Iran kuwa, mataifa ya Magharibi yanapaswa kuiondolea Urusi vikwazo vya uuzaji wa nafaka zake.
Vita vya nchini Ukraine vimeathiri pakubwa usafirishaji wa ngano na nafaka nyengine duniani na kuzua hofu ya kutokea uhaba wa chakula.