Urusi yawasajili Waafrika kutengeza droni za vita Ukraine
10 Oktoba 2024Wanawake hao wanafanya kazi katika kiwanda kinachohusika kuunda maelfu ya droni za Iran zinazotumika kuishambulia Ukraine.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti maalumu iliyotolewa na shirika la habari la Associated Press baada ya kukamilisha uchunguzi wake.
Katika mahojiano ya shirika la habari la AP baadhi ya wanawake wamesema walilaghaiwa kwamba wanakwenda Urusi katika programu ya kufanya kazi na kusoma. Badala yake wameeleza kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu wakiwa chini ya uangalizi muda wote.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa, Urusi inayokabiliwa na uhaba wa nguvukazi katika kipindi hiki cha vita, kupitia Abaluga, imewaajiri wanawake kutoka Uganda, Rwanda, Kenya, Sudan Kusini, Sierra Leone na Nigeria, pamoja na Sri Lanka iliyo Kusini mwa bara la Asia.