SiasaUkraine
Maelfu ya watu wakimbia Kharkiv kutokana na mashambulizi
13 Mei 2024Matangazo
Gavana wa Kharkiv Oleg Syniehubov amesema zaidi ya watu 4,000 wamehamishwa na kwamba "maeneo yote" yaliyo mpakani na Urusi yanashambuliwa.
Mamlaka imeripoti vifo vya raia kadhaa katika mashambulizi hayo, kifo cha hivi karibuni kikiwa cha mzee wa miaka 63 aliyeuawa kazika kijiji cha Glyboke.
Soma pia: Watu 17 wajeruhiwa katika shambulizi la Ukraine nchini Urusi
Mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskii amekiri kuwa vikosi vyake vinakabaliwa na "wakati mgumu" japo wanaendelea kukabiliana na wanajeshi wa Urusi.
Tangu mwezi Machi, Urusi imezidisha mashambulizi nchini Ukraine na kulenga miundombinu ya nishati na makaazi ya watu.