Urusi yazitahadharisha meli zinazopitia Bahari Nyeusi
20 Julai 2023Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imesema vyombo hivyo vinavyoelekea kwenye bandari za Ukraine vitazingatiwa na Moscow kuwa vimebeba shehena ya silaha na mataifa yanayozimiliki yatakuwa yamejiingiza kwenye vita vya Ukraine na yapo upande wa serikali ya Kyiv.
Tamko hilo la Urusi linafuatia uamuzi wake wa siku ya Jumatatu wa kujitoa kutoka mkataba wa kusafirisha nafaka za Ukraine kupitia bandari za Bahari Nyeusi.
Ukraine kwa upande wake imezirai nchini nyingine kwenye kanda ya Bahari Nyeusi kuingilia kati na kuhakikisha usalama wa meli zote zinazotumia ujia huo wa maji.
Serikali ya rais Volodymyr Zelensky imeituhumu Urusi kuwa inalenga kuhujumu kwa makusudi miundombinu ya usafirishaji wa nafaka na mazao mengine ya chakula na kuyaweka hatari mataifa yenye uhitaji duniani