Urusi yazuia shambulizi kubwa la droni huko Moscow
21 Agosti 2024Matangazo
Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin amesema leo kuwa hilo ni moja kati ya mashambulizi makubwa kuwahi kutokea kwenye mji wa Moscow kwa kutumia droni. Sobyanin amesema hakuna uharibifu au majeruhiwa wowote ambao wameripotiwa. Wakati huo huo, vikosi vya Ukraine vimesema vimeushambulia mfumo wa kujikingana makombora aina ya S-300 uliopo kwenye jimbo la Rostov, kusini mwa Urusi. Uongozi wa jeshi la Ukraine umesema shambulizi hilo limetokea karibu na Novoshakhtinsk, na kwamba mifumo ya S-300 ilitumika kushambulia miundombinu ya kiraia nchini Ukraine. Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev amesema leo kuwa hapatokuwa tena na mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine, baada ya Kiev kulivamia jimbo la Kursk nchini Urusi.