1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

US, UK, EU wataka uchunguzi kuhusu uchaguzi wa Pakistan

10 Februari 2024

Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kwa nyakati tofauti wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na mchakato wa uchaguzi nchini Pakistan na kutoa wito wa uchunguzi wa madai yaliyoripotiwa ya udanganyifu.

https://p.dw.com/p/4cFTI
Pakistan | Uchaguzi wa mwaka  2024
Maafisa wa Pakistan wakihesabu kura mjini Lahore katika Uchaguzi wa mwaka 2024Picha: Navesh Chitrakar/REUTERS

Marekani na Umoja wa Ulaya wameyataja madai ya uingiliaji, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wanaharakati na kuongeza kuwa madai hayo ya udanganyifu na rushwa yanatakiwa kuchunguzwa.

Soma pia: Washirika wa Imran Khan waongoza uchaguzi Pakistan

Taarifa ya Umoja wa Ulaya imesema hakukua na usawa, ikiwaangazia wanasiasa waliozuiwa kugombea pamoja na kuwazuia watu kukusanyika, uhuru wa kujieleza na kuzuia huduma za intaneti.

Pakistan ilifanya uchaguzi wa bunge la kitaifa lenye viti 265 na chama kimoja kinahitaji viti 133 ili kupata wingi wa kutosha.