Usafiri wasimama Tunis, kufuatia mgomo wa watumishi
2 Januari 2023Wafanyakazi hao wamegoma kutokana na ucheleweshwaji wa malipo na marupurupu.
Msemaji wa kampuni hiyo ya usafiri Hayat Chamtouri, amesema muungano wa wafanyikazi unapinga kucheleweshwa kwa malipo na marupuru ya wafanyikazi.
Mgomo huo umeweka wazi matatizo ya kifedha yanayozikabili kampuni za umma ambazo ziko ukingoni mwa kufilisika, wakati serikali ya Rais Kais Saied ikiwa inakumbwa na mzozo mbaya wa kifedha.
Mgomo huo wa usafiri ni ishara ya nguvu ilizo nazo muungano huo wa wafanyikazi wa UGTT, ambao umeahidi kuendelea kuishinikiza serikali.
Muungano huo wa wafanyikazi, wenye wanachama milioni 1, umeidhinisha siku mbili za mgomo katika sekta ya uchukuzi ikiwemo safari za ndege, nchi kavu na baharini kuanzia Januari 25 na 26, ili kupinga kile walichokiita "serikali kutelekeza baadhi ya kampuni za umma."