Dunia inazalisha taka za plasitiki tani mil. 57 kila mwaka
5 Septemba 2024Utafiti mpya uliochapishwa na Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza, unaonyesha kuwa dunia inazalisha kiasi cha tani milioni 57 za taka za plastiki kila mwaka. Taka hizo zinasambaa kutoka baharini, milimani na hadi ndani ya miili ya watu. Kulingana na utafiti huo, mji wa Lagos nchini Nigeria ndio ulizalisha taka nyingi za plastiki kuliko jiji lolote. Miji mingine mikubwa zaidi inayozalisha taka za plastiki ni New Delhi, Luanda, Angola; Karachi, Pakistan na Al Qahirah, Misri.
Soma: Viongozi wajadili mkataba wa taka za plastiki
India inaongoza duniani kwa uchafuzi wa plastiki, ikizalisha tani milioni 10.2 kwa mwaka, mara mbili zaidi ya mataifa makubwa yanayofuata katika uchafuzi wa mazingira, Nigeria na Indonesia. China, ambayo mara nyingi imeharibiwa na uchafuzi wa mazingira, inashika nafasi ya nne lakini inapiga hatua kubwa katika kupunguza taka.