1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Idadi ya wagongwa wa kisukuri imeongezeka duniani

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2024

Utafiti wa hivi karibuni wa jarida la The Lancet unaonyesha kuwa idadi ya watu wazima wanaougua kisukari duniani kote imeongezeka maradufu katika miongo mitatu iliyopita, huku ongezeko kubwa ni katika nchi zinazoendelea.

https://p.dw.com/p/4mxYh
Vipimo vya kisukari
Vipimo vya kisukariPicha: Peter Byrne/empics/picture alliance

Utafiti wa hivi karibuni wa jarida la Lancet unaonyesha kuwa idadi ya watu wazima wanaougua kisukari duniani kote imeongezeka maradufu katika miongo mitatu iliyopita, huku ongezeko kubwa likishuhudiwa katika nchi zinazoendelea.

Utafiti unabainisha kwamba tatizo la kisukarilimeathiri karibu asilimia 14 ya watu wazima duniani kote kufikia mwaka 2022, ikilinganishwa na asilimia saba mwaka wa 1990. Zaidi ya watu milioni 800 duniani sasa wanaugua kisukari.

Watafiti wamesisitiza kuwa unene kupita kiasi ni sababu kubwa inayochangia kisukari aina ya 2 huku pengo la kutibu ugonjwa huo baina ya nchi tajiri na maskini pia likiongezeka.

Mwandishi mkuu wa utafiti huo Majid Ezzati wa Chuo cha Imperial London alisema kuwa kukosekana kwa matibabu thabiti kunahatarisha matatizo mengine ya kiafya kwa watu wenye umri mdogo haswa katika nchi zenye kipato cha chini.