1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utulivu warejea Kampala baada ya miripuko ya bomu

17 Novemba 2021

Huku kundi la IS likidai kufanya mashambulio ya mabomu mjini Kampala, polisi imeendelea kufuatilia mtandao wa kundi la waasi wa ADFambao wanaendesha harakatai zao za itikadi mashariki ya Congo

https://p.dw.com/p/436c2
Uganda nach den Bombenanschlägen in Kampala
Picha: Lubega Emmanuel/DW

Hata hivyo hali imerejea kuwa ya kawaida mjini Kampala, huku idadi ya waliopoteza maisha ikiongezeka. Hii ni kutokana na baadhi ya waliojeruhiwa vibaya kufariki hospitalini.

Soma zaidi: Watu 6 wauawa, 33 wajeruhiwa kwenye miripuko Kampala

Kundi la IS limedai kwamba linaendesha mashambulizi Uganda kutokana na taifa hilo kuhusika katika harakati ya kukabiliana nao huko Afrika ya Kati. Katika ujumbe wake aliosambaza kwa vyombo mbalimbali vya habari, rais Museveni amendelea kulikosoa kundi la waasi wa Allied Democratic Front ADF kwa vitendo hivyo vya kuwashawishi vijana kujitoa mhanga. Amewataka viongozi wa ADF wenyewe wadiriki wajiripue wenyewe kudhihirisha kuwa kile wanachofanya ni sawa. Kwa mujibu wa taarifa za polisi, kundi la ADF ndilo linaendesha mashambulio ya mabomu Uganda. 

Uganda Explosion in Kampala
Miripuko hiyo imewauwa watu wanne mpaka sasaPicha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Polisi ilimkamata mwanamume mmoja ambaye inadaiwa alikuwa miongoni mwa magaidi waliotekeleza mashambulio kwenye kituo kikuu cha polisi cha Kampala na eneo la bunge. Hata hivyo aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwaongoza hadi kwake nyumbani walikopata vifaa kadhaa vya kutengeneza mabomu. Mauaji yake yameibua mjadala mkubwa,baadhi ya wananchi wakisema kuwa hatua bora ingekuwa kuendelea kumhoji ili aelezee zaidi kuhusu sababu za kundi lao kuendelea kusababisha vifo vya raia wasio na hatia.

Soma zaidi: Miripuko miwili yaitikisa Kampala

Kwingineko, watu 36 walionusurika na kupata majeraha wanaendelea kupata matibabu. Ila kutokana na hali mahututi walimokuwa baadhi yao, kuna mashaka kuhusu baadhi yao kama watapona. Mmoja amefariki hii leo. Daktari mkuu wa polisi Moses Byaruhanga amefafanua kuwa walipokea miili ya watu sita pamoja na vipandevipande vya vyungo ambavyo bado wanachunguza ni vya nani. 

Huku viongozi mbalimbali duniani wakiendelea kulaani mashambulio hayo ya siku ya Jumanne asubuhi, hali ya utulivu imereja katika mji wa Kampala. Hata hivyo watu wengi wamechukua tahadhari kutokwenda maeneo yenye misongamano. Kinyume na matarajio kwamba bunge lingerejelea vikao vyake leo, naibu wa spika ameviahirisha hadi kesho. Bomu la pili liliripukia jirani na bunge na waheshimiwa kadhaa wamelezea kuwa magaidi walikuwa wanawalenga. Eneo hilo lingali marufuku kwa umma wakati uchunguzi ukiendelea kufanywa.

Lubega Emmanuel DW Kampala