Serikali ya Uturuki imeushambulia kwa ndege mji wa Kurdistan
19 Julai 2019Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar alisema shambulio hilo ni kulipiza kisasi baada kuuliwa kwa balozi huyo mdogo kwa kupigwa risasi akiwa mkahawani. Duru kutoka kikosi cha polisi zinaeleza kwamba watu wengine wawili pia wamefariki baada ya kushambuliwa katika tukio hilo. Hulusi ameeleza kwamba kufuatia shambulizi ovu lililotokea katika eneo la Arbil wameanzisha mashambulizi makali ya angani katika eneo la Qandil na kushambulia kwa nguvu muungano wa kundi la kigaidi la PKK.
Katika taarifa yake Hulusi alieleza kwamba wamevishambulia na kuviharibu vituo vya silaha, majengo ya kulala na mapango yanayotumiwa na magaidi huku akieleza kwamba wataendelea kuongeza mashambulizi hadi makundi ya kigaidi yatakapomalizwa nguvu na vile vile kulipiza kisasi cha damu iliyomwagika.
Katika shambulizi la risasi la Jumatano hakuna kundi limedai kuhusika ila wataalamu wengi wa Iraq wameeleza uwezekano wa kuhusika kwa Chama cha Wakuridistan wanaoataka kujitenga cha PKK, Chama ambacho serikali ya Uturuki pamoja na Umoja wa Ulaya wanakitambua kama kundi la kigaidi baada ya miongo mitatu ya kuishambulia Utruki. Uturuki imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya makusudi katika mkoa wa Kazkazini kwa lengo la kuwamaliza wanachama wa PKK ambao wamekuwa wakiishambulia Uturuki tangu mwaka 1984. Msemaji wa PKK amekanusha kundi hilo kuhusika na shambulizi la Jumatano.
Chama cha KDP kinaongoza mkoa wa Kazkazini
Mapema mwezi huuu chama cha PKK kilitangaza kwamba katika mashabulizi hayo kiongozi mwanadamizi wa PKK Diyar Gharib Mohammed aliuwawa pamoja na wapiganaji wengine wawili. Kwa sasa chama cha Demokrasia cha Kurdistan, KDP, kilicho na uhusiano mzuri wa kisiasa na biashara na serikali ya Uturuki ndicho kinachoongoza mkoa huo wa Kazkazini.
Kulingana na shirika la habari la Uturuki, mtu mmoja aliyekuwa na bunduki mbili aliingia katika mkahawa na kuwafyatulia risasi na kumuua balozi huyo mdogo wa Uturuki na raia mwengine wa Iraq na kuwajeruhi wengine. Hadi sasa mshambuliaji huyo hajakamatwa licha ya polisi kuweka vizuizi mjini humo na nje ya mji. Msemaji wa raisi wa Uturuki, Ibrahim Kalin aliapa kwamba hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya waliotekeleza shambulizi hilo baya.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq umetaka pande zote mbili kujizuia dhidi mashambulizi zaidi.
(AFPE)