1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yataka kumaliza mvutano na Umoja wa Ulaya

Saleh Mwanamilongo
7 Julai 2020

Uturuki imeuomba Umoja wa Ulaya kuwa mpatanishi katika mzozo baina yake na nchi wanachama wa umoja huo ikiwemo Ufaransa. Waziri wa mambo ya Nje wa Uturuki amezungumza na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/3ev1d
Türkei | PK | Mevlut Cavusoglu - Josep Borrell Fontelles in Ankara
Picha: picture-alliance/AA/C. Ozdel

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki,Mevlut Cavusoglu, anasema Uturuki iko tayari kujibu kwa hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi yake na Umoja wa Ulaya. Kwenye mkutano wa pamoja na waandishi habari kufuatia ziara ya mkuu wa sera za nje na usalama wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrel, Cavusoglu alitoa mwito kwa Ufaransa wa kuomba msamaha kwa Uturuki kutokana na mkwaruzano wa meli za nchi mbili hizo kwenye bahari ya Mediterania.

Mahusiao baina ya mataifa hayo washirika katika jumuiya ya kujihami ya NATO yamechafuka katika wiki za hivi karibuni kuhusiana na suala la Libya na utafutaji mafuta na gesi katika eneo la mashariki mwa bahari ya Mediterania. Kufuatia tukio hilo, Ufaransa ilisitisha ushiriki wake katika operesheni ya majini ya jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya katika Bahari ya Mediterania inayolenga kusaidia kutekeleza marufuku ya biashara ya silaha dhidi ya Libya.

Frankreich Paris | Staatstreffen | Erdogan und Macron
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan(kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: picture-alliance/AP Photo/L. Marin

Ziara hiyo ya Borrel imekuja wakati ambapo kunazuka tofauti nyingi baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki kuhusu maswala kadhaa, ukiwemo mzozo baina ya Uturuki na Ugiriki pamoja na Cyprus kuhusu mashariki mwa bahari ya Mediterania. Umoja wa Ulaya unalenga kuiwekea vikwazo Uturuki.

Tunataka kufanya kazi na Umoja wa Ulaya,alisema waziri wa mambo ya nje wa Uturuki,lakini ikiwa EU itaiwekea vikwazo Uturuki tutalakizimika kulipiza.Na mzozo utakuwa mkubwa na hauta saidia mtu yoyote.

Cavusoglu amesema kwamba wanasubiri kuona UE kutoegemea upande wowote na kuchangia katika suluhisho la mzozo baina yake na Ugiriki pamoja na Cyprus.

Europa Symbolbild Flüchtlingsboot auf dem Mittelmeer
Boti iliyowabeba wakimbizi kutoka Uturuki ikikaribia bandari ya Thermi UgirikiPicha: Imago Images/Xinhua/M. Lolos

Uturuki ilipeleka meli zake za kijeshi kwenye eneo la uchimbaji wa gesi ambako Cyprus inasema kwamba ni eneo lake. Serikali ya Uturuki ilisema kwamba hatua yake ni kwa ajili ya kuyalinda maslahi yake na ya Cyprus. Serikali ya Cyprus imeituhumu Uturuki kwa kuvamia maji yake kwenye Bahari ya Mediterania Mashariki. Kuhusu swala hilo, Umoja wa Ulaya unaunga mkono misimamo ya Ugiriki na Cyprus.

Hata hivyo, Josep Borrel alisema kwamba Uturuki ni mshirika muhimu wa Umoja wa Ulaya, licha ya kwamba uhusiano hivi sasa umekuwa mgumu. "Asante kwa mapokezi na nafasi hii ya kwanza ya kuzungumzia maswala mengi. Hali mashariki ya Mediterania ,hali ya kikanda huko Libya na Syria. Tunatakiwa kufanya kazi pamoja ili kuyaboresha", alisema Borrel.

Borrel ameomba kuweko na uhusiano na mazungumzo zaidi.

Uturuki imeingilia katika wiki za hivi karibuni nchini Libya ikitoa usaidizi wa anga,silaha na wapiganaji kutoka Syria kuisaidia serikali inayotambuliwa kimataifa mjini Tripoli.