Uwindaji haramu tishio kwa wanyamapori
10 Juni 2011Matangazo
Watalii wengi huvutiwa kuzitembelea nchi za Afrika ya Mashariki kutokana na urithi wa mbuga zake zenye wanyama wa kila aina. Lakini kwa siku za karibuni, uwindaji haramu wa wanyama hao umekuwa ukiongezeka na sasa serikali zinahofia kupoteza mapato ya utalii na pia kuhatarishwa kwa mfumo wa uhusiano wa kimaumbile kati ya wanyama, wanaadamu na mimea.
Makala hii ya Mtu na Mazingira inaangazia kwa undani suala hilo.
Mtayarishaji/Msimulizi: Rose Athumani
Mhariri: Othman Miraji