Vettel anafikiriwa kuwa dhaifu isivyo, asema Ecclestone
10 Aprili 2019Mjerumani huyo aliyeshinda mbio za F1 mara nne na kampuni ya Red Bull amepambana kupata uthabiti tangu alipohamia Ferrari mwaka 2015.
Mpaka sasa mwaka huu amemaliza katika nafasi ya nne nchini Australia na ya tano nchini Bahrain baada ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda taji kabla ya kuanza kwa msimu.
Mashindao ya China grand Prix yanayofanyika Jumapili ijayo yatakuwa kipimo kikubwa lakini Ecclestone amemuunga mkono dereva huyo mwenye umri wa miaka 31.
"FormulaOne inamhitaji Sebastian anayeshinda," amesema Ecclestone mwenye umri wa miaka 88 katika mahojiano na magazeti ya Sport Billd na Auto Bild Motorsport.
"Ana kinasaba cha ushindani ambacho madereva wengi walikuwa nacho," aliongeza Muingereza huyo. "Watu wanamfikiria isivyo Sebastian kuwa dhaifu."
Vettel tayari ana alama 22 nyuma ya kinara Valtteri Bottas na alama 21 nyuma ya bingwa mtetezi Lewis Hamilton, ambao wote wanaendesha magari ya Mercedes.
"Atapambana kujitoa katika matatizo yanayomkabili hivi sasa," Ecclestone aliongeza.
Hakuna sababu kwa nini sambamba na Lewis, Sebastian hawezi kufikia rekodi ya mataji saba aliyoiweka Michael Schumacher."