1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Video kufanyiwa majaribio katika kandanda

4 Juni 2016

Bundesliga ni miongoni mwa ligi sita ambazo zitaufanyia majaribio mfumo wa matumizi ya waamuzi wasaidizi wa kutumia video yaani Video Assistant Referees - VARs.

https://p.dw.com/p/1J0d9
Fußball Premier League Reading - Noriwch City
Picha: picture alliance/empics

Rais wa FIFA Gianni Infantino anatumai kuwa mfumo huo mpya utaweza kufanya kazi kikamilifu katika Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi.

Bodi ya kimataifa ya kandanda – IFAB imesema ligi za nchini Australia, Brazil, Ujerumani, Ureno, Uholanzi na Marekani ndizo za kwanza kuyakubali masharti yaliyowekwa na IFAB na FIFA kushiriki katika majaribio ya waamuzi wasaidizi wa kutumia video.

FIFA imesema majaribio ya mwanzo yatawapa tu fursa waamuzi waisaidizi wa kutumia video kujifahamisha na mfumo huo kutathmini namna ambavyo wanaweza picha zinavyoweza kurudiwa tena na tena huku wakijifunza namna ya kutoa maamuzi kuhusu matukio ya wazi yanayoweza kuubadilisha mchezo lakini bila kuwasilisiana na refarii. Katika awamu hii michuano haitaathirika na maamuzi yao.

Chini ya mpango huu, picha za video zinazorudiwa tena na tena zitatumiwa katika kufanya maamuzi kuhusu mabao, uwezekano wa penalti, kuwapa kadi nyekundu wachezaji au katika matukio ya kumwadhibu mchezaji ambaye siye.

Hadi sasa, teknolojia imetumika tu kwa maamuzi ya kama mpira umevuka mstari wa lango, mfumo ulioanzishwa na FIFA katika Kombe la Dunia la 2012 nchini Japan.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu