1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya maporomoko ya udongo Uganda vyafikia watu 28

4 Desemba 2024

Idadi ya watu waliokufa katika maporomoko ya udongo mashariki mwa Uganda imeongezeka na kufikia 28, baada ya miili zaidi ya watu kupatikana ikiwemo wavulana wawili wa umri wa miaka mitatu.

https://p.dw.com/p/4nisA
Uganda | Erdrutsch in Bulambuli
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu Uganda wakitafuta miili baada ya maporomoko ya udongo kufuatia mvua kubwa iliyoziba nyumba 40 katika wilaya ya milimani ya Bulambuli, mashariki mwa Uganda,Novemba 28, 2024.Picha: Nakasiita/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo kufuatia maporomoko hayo yaliyotokea Jumatano iliyopita katika mteremko wa mlima Elgon uliopo mpakani na Kenya.Tangu wakati huo miili zaidi imepatikana ikiwemo ya wavulana wawili, hii ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa ya polisi waliyoitoa Jumatatu jioni bila kueleza zaidi. Tangu mwezi Oktoba, mvua kubwa zisizo za kawaida zimesababisha mafuriko na maporomoko ya udongo katika baadhi ya maeneo ya Uganda.