Kundi la Kombgreen linaloundwa na vijana ambao zamani walikuwa wahalifu katika mtaa wa Korogocho jijini Nairobi, wameweka juhudi zao pamoja na kutengeneza bustani kwenye kingo za mto Nairobi. Bustani hiyo iliyo karibu na daraja la Korogocho, hivi sasa ni kivutio kwa watu wengi wanaotaka kujipumzisha. Sikiliza makala hii ya Mtu na Mazingira iliyotengenezwa na Thelma Mwadzaya.