Kaunti ya Kwale ni moja ya kaunti za pwani ya Kenya ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari kuhusu idadi kubwa ya vijana wanaodaiwa kuwa hujiunga na makundi ya kigaidi na pia kupokea mafunzo ya itikadi kali. Hata hivyo Shirika lisilo la kiserikali la Smartmove Community limepiga hatua kubwa katika kubadilisha misimamo mikali ya baadhi ya vijana.