1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Iraq vyasema vimemuua kiongozi wa kundi la ISIS

22 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani ametangaza hii leo kuwa kiongozi wa kundi linalojiita dola la kiislamu la ISIS aliuawa katika operesheni ya kijeshi pamoja na viongozi wengine wa kundi hilo.

https://p.dw.com/p/4m6MF
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al-Sudani
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al-SudaniPicha: Murtadha Al-Sudani/Anadolu Agency/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu huyo alisema kiongozi wa kundi la ISIS anayefamika kama Jassimal-Mazroui Abu Abdul Qader aliuawa katika operesheni maalum ya vikosi vya kukabiliana na ugaidi chini ya kamandi ya kijeshi ya pamoja katika milima ya Hamrin katika mkoa wa Salahuddin.Muungano wa zaidi ya nchi 80, ukiongozwa na Marekani, uliunda kikosi cha kupambana na kundi hilo la dola la kiislamu ambalo lilipoteza udhibiti wake wa maeneo ya Iraq 2017 na Syria mwaka 2019 ingawa bado kumekuwepo na mashambulizi ya kundi hilo ya hapa na pale.Mwezi uliopita, Marekani ilitangaza makubaliano na serikali ya Iraq kukamilisha tume ya muungano huo wa kijeshi baada ya muongo mmoja.