Vikosi vya kijeshi vya Ukraine na Urusi vyaendelea kupambana
6 Januari 2025Matangazo
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimeukamata mji wa Ukraine wa Kurakhove ambao ni kituo muhimu kwa vikosi vya Ukraine kupata vifaa na msaada wa vifaa vya kiufundi. Mafanikio makuu ambayo vikosi ya Ukraine imeyapata katika katika kipindi cha miezi mitano ya mapigano yamekuwa kukamata na kushikilia kipande cha eneo ndani ya eneo la Kursk la Urusi. Hapo jana Mkuu wa ofisi ya rais nchini Ukraine, Andriy Yermak alipokuwa akielezea mashambulizi mapya huko Kursk, amesema Urusi "itakipata inachostahili". Pande zote mbili zinapigana ili kusonga mbele katika uwanja wa mapambano siku chache kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump hapo Januari 20. Trump aliahidi atavimaliza vita hivyo kwa haraka.