Vikosi vya Ukraine vyajipenyeza ndani ya Urusi
8 Agosti 2024Matangazo
Kaimu Gavana wa mkoa wa Kursk, Alexey Smirnov, ametangaza hali ya hatari kwenye mkoa huo wa mpakani unaotambulika kuwa kituo kikuu cha usambazaji gesi asilia.
Wizara ya afya ya Urusi imesema raia 31, wakiwemo watoto sita, wamejeruhiwa, huku Gavana Smirnov akisema watu watano wameuawa kufikia sasa.
Jeshi la Urusi linasema limeimarisha ulinzi kuzunguka kinu cha umeme wa nyuklia na mitambo yake minne kwenye mkoa huo wa Kursk.
Licha ya mafanikio hayo, Ukraine imepoteza eneo lenye ukubwa wa kilomita 420 za mraba tangu katikati ya mwezi Juni mwaka huu.