1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Umoja wa Afrika - Darfur.

O.Mutasa23 Mei 2007

Jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda Amani eneo la Darfur magharibi mwa Sudan bado linajivunia kazi linayoifanya huko licha ya Jeshi hilo kukumbwa na matatizo kadha ya kifedha na pia kushindwa kudhibiti hali ya mambo.

https://p.dw.com/p/CHDr
Mapigano yaendelea Darfur
Mapigano yaendelea DarfurPicha: picture-alliance /dpa

Badhi ya repoti zinasema Jeshi hilo huenda sasa likashindwa kudumisha Amani Darfur na kujitoa katika shughuli hio.

Inaarifiwa kua jeshi la Umoja wa Afrika liloko Darfur lenye Askari 7000 wengi ya wanajeshi hao hawajapokea mshahara wao kwa muda wa miezi mi nne , hii imewafanya wanajeshi hao kushindwa hata kununua sigareti au kuwasiliana na jama zao kwa njia ya simu.

Huu ni mwaka wa tatu sasa ,jeshi hilo la Afrika likiwa Darfur ,eneo ambalo zaidi ya watu Mia mbili Elfu wamesha uawa kutokana na mapigano baina ya vikosi vya Askari wa Janjawid na waasi wa kundi la Vuguvugu la ukombozi wa Sudan (Sudan Liberation Movement)

Huku zaidi ya watu Millioni mbili wakikimbia makazi yao tangu machafuko hayo yaanze miaka mi nne iliopita.

Akizungumza na shirika la Habari la kifaransa AFP, Hassan Gibril Alieu, kiongozi wa pili wa jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda Amani Darfur,

amekubali kuepo matatizo katika kikosi hicho cha Umoja wa Afrika ,lakini Hassan Gibril anakanusha repoti za vyombo vya Habari vya Marekani kua nchi za Afrika zilizo jitolea kuchangia wanajeshi wake huko Darfur; sasa zinajianda kuyaondoa majeshi yao.

Jeshi hili la Umoja wa Afrika tayari wanajeshi wake 19 wamesha uawa.

Mwezi jana mapigano yalitokea kaskazini mwa Darfur karibu na mpaka wa Chad, ambapo Askari watano wakulinda Amani kutokea Senegal walipoteza maisha yao, huku waasi wawili wa Sudan Liberation Movement pamoja na raia moja wa Sudan nao kufariki kwenye mapigano hayo.

Serekali ya Senegal inadai kifo cha Askari wake kilitokana na kundi la SLM kundi peke la Darfur ambalo lilifanya mkataba wa Amani na Serekali ya Sudan.

Lakini viongozi wa Jeshi la AU walisema, kitendo hicho cha kuwawa Askari jeshi wa Senega,l ilikua ni kazi ya Shetani wakiogopa kutoa lawama ya moja kwa moja kwa kundi la SLM wengi ya wafasi wake wakiwa kabila la Zaghawa.

Magari 100 ya jeshi hilo la AU yameibwa na kulifanya jeshi hilo kushindwa kufanya kazi ya kupiga Doria eneo la Darfur lenye ukubwa ,sawa na nchi ya Ufaransa.

Jeshi la AU lilikua lipate usaidizi wa magari ya diraya 36, pamoja na Helikopta za kivita 6 kutoka Umoja wa Mataifa na pia kuongeza jeshi la watu Elfu tatu ,yote hayo huenda yasiwezekana kutokana na Serekali ya Khartoum kulikatalia jeshi la Umoja wa mataifa (UN) kuchukua nafasi ya jeshi la Umoja wa Afrika kwenye eneo la Darfur .UN imetaka kwa jumla kutuma Askari Elfu 20 wakulinda Amani eneo la Darfur .

Mohd Ahmed moja ya wakimbizi walioko kwenye kambi ya As-Salam yenye watu Elfu Arubaini na tano (45)

nje kidogo ya mji mku wa Dafur, El Fasher, alilamika kua, hapana lenye kutatuliwa panapotokea mapigano;

Makamanda wa jeshi la AU hutumia ttu njia za kidiplomasia kujaribu kutuliza mambo,na sheria haiwaruhusu kuingilia kati mapigano yanapotokea ispokua kujilinda wao ,wala jeshi la AU halina uwezo wa kushuritisha au kuzishinikiza pande zinazopigana kukubali mpango wa Amani.

Lakini Kamanda Hassan Gibril alisema, matatizo ya watu wa Darfur yangekua makubwa zaidi lau jeshi la Umoja wa Afrika lisingekueko huko.

Nawao kama jeshi la AU wanajivunia kazi yao wanayoifanya huko Darfur.