Vikwazo vyainyemelea Niger
30 Julai 2023Kwenye mkutano huo wa kilele huenda viongozi hao wakaukabiliana kuiwekea vikwazo Niger.
Kabla ya mkutano huu wa leo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alizungumza na rais wa Nigeria Bola Tinubu akielezea wasiwasi wake juu ya hali nchini Niger na kusisitiza kuendelea kuunga mkono juhudi za kiongozi huyo za kurejesha utawala wa kikatiba.
Rais aliyechaguliwa wa Niger Mohamed Bazoum amekuwa akizuiwa na jeshi kwa siku nne, na tayari Jenerali Abdourahamane Tiani, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais amejitangaza kuwa kiongozi wa taifa hilo.
Tinubu ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo kwa mataifa ya Afrika ya Magharibi, ECOWAS amesema jumuiya hiyo na ya kimataifa wanafanya kila linalowezekana kuilinda demokrasia ya Niger.