Vilabu vya Bundesliga vitafanya vipi katika msimu wa 2017-18?
Nani atashinda Taji la Bundesliga, nani ataingia Kinyang'anyiro cha Mabingwa, nani atafika kwenye Mabingwa wa Uropa na nani atashushwa daraja? Ufuatao ni utabiri wetu jinsi timu 18 za Bundesliga zitakavyochuana 2017-18.
Bayern Munich
Katika ligi ya Bundesliga, timu 18 hucheza mechi 34 kila moja na mara nyingi Bayern Munich huibuka washindi wa taji. Imeshinda mara 27. Baada ya kumnunua Corentin Tolisso kwa kima cha euro milioni 40, ambacho ni juu zaidi katika historia yake, azma ya mabingwa hawa wa Ujerumani inasalia ile ile, kutwaa taji. DW inabashiri kuwa Bayern pekee ndiyo inaweza kutwaa taji la Bundesliga msimu huu.
RB Leipzig
Timu hii ambayo ni ngeni katika Bundesliga ilishindana vikali na Bayern msimu uliopita hadi ikaingia katika Kinyang'anyiro cha Mabingwa. Sasa watashiriki mashindano 3: Je, watashikilia falsafa yao ya kuwakuza wachezaji wachanga? Je, watastahimili kishindo cha Europa? Ubashiri wa DW: Itamaliza miongoni mwa 5 bora lakini hakuna uhakika wa kupata tiketi ya moja kwa moja kuingia Kombe la Mabingwa.
Hoffenheim
Kocha mwenye umri mdogo zaidi katika Bundesliga aliiongoza Hoffenheim kuingia Kombe la Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. Katika kusonga mbele, matarajio ni tele kwa timu hii. Nagelsmann ambaye alitawazwa Kocha bora wa mwaka ni mweledi na timu zake huwa zimejiandaa vyema. Swali linaloikumba Leipzig ndilo pia linaikumba Heffenheim. Ubashiri wa DW: Itamaliza kati ya 5 bora.
Borussia Dortmund
Msimu uliopita ulikuwa wa aina yake! Vurugu za mashabiki, basi lao kushambuliwa na kocha kutimuliwa. Kocha mpya, Peter Bosz, atarajiwa kuiongoza timu hii na labda ishinde ligi. Timu alizofunza za Ajax huwa na mchezo wa kasi na wa kushambulia upesi, mbinu zinazopendwa pia na Johan Cruyff. Utabiri wa DW: BVB itamaliza kati ya timu 3 bora ikiwa Pierre-Emerick Aubameyang na Mario Götze hawatajeruhiwa.
1. FC Köln
Kwa mara ya kwanza katika miaka 25, Cologne wamerejea katika ubingwa wa Ulaya. Hata hivyo kashfa kuhusu kuondoka kwa Antony Modeste imepunguza nguvu za klabu hii. Haijulikani vipi itafaulu bila mshambuliaji wao aliyefunga mabao 25 katika ligi na katika bara. Hata hivyo, wangali katika mikono salama ya kocha Peter Stöger. Utabiri wa DW: Hawawezi wakapanda zaidi ya nafasi ya katikati kwenye jedwali.
Hertha Berlin
Kikatuni cha bahati cha Hertha, Herthinho, kinaonekana kufurahishwa na ziara ya timu yake Ulaya. Wakati kama huu msimu uliopita, klabu ilikuwa imeshatolewa nje ya Ligi ya Europa. Lakini msimu huu, timu hii itafanya angalau ziara 3 za nje kuchuana. Hilo linaathiri vipi nafasi zake katika Bundesliga? Utabiri wa DW: Timu nyingine ni imara zaidi, hivyo kufaulu tena kwenda Ligi ya Europa si rahisi.
Freiburg
Ndoto yao ya kushiriki Ligi ya Europa ilitoweka hata kabla haijaanza. Freiburg ilitolewa nje katika awamu ya kufuzu kwa Ligi ya Europa pale iliposhindwa na Domzale ya Slovenia. Kwa mara nyingine sasa, kocha Christian Streich analenga kufuzu kwenye Kombe hilo. Ubashiri wa DW: Hawatafaulu kwa sababu hakuna timu ambayo ni dhaifu kuliko walivyokuwa msimu uliopita.
Werder Bremen
Kipindi hiki cha uhamisho unaofungamana na msimu wa jua, Werder ilimsajili mchezaji wa kwanza kutoka China, Yuning Zhang. Lakini hataweza kujaza mapengo ambayo yameachwa na mlinda lango Felix Wiedwald, nahodha Clemens Fritz na Claudio Pizarro, ambao wameondoka. Utabiri wa DW: Bremen itashuka nafasi kadhaa chini kwenye jedwali lakini pia itawavutia baadhi ya mashabiki wapya kutoka Mashariki.
Borussia Mönchengladbach
Je, timu hii inahitaji baraka kutoka kwa Papa? Baada ya kumaliza katika nafasi ya 9 msimu uliopita ambayo ni ya kusikitisha, haiwezi ikarudia hali hiyo ya kuvunja moyo. Japo haiwezi ikashindana kifedha na Bayern, Dortmund ama Leipzig, lakini je inaweza kushindana uwanjani? Utabiri wa DW: Hawatafikia Kombe la Mabingwa, lakini labda Ligi ya Europa.
Eintracht Frankfurt
Ni nini Eintracht Frankfurt inafanya na kifaa cha kukausha mikate? Tazama hapa: Katika nusu ya kwanza ya msimu uliopita, Eintracht ilivutia kama silesi ya mkate iliyokaushwa vizuri pale walipokuwa namba 2. Lakini mwisho wa msimu, walikuwa kama silesi iliyoungua! Msimu huu nia yao ni kuingia Ligi ya Europa. Utabiri wa DW: Hawataweza - Watapata changamoto kuanzia mwanzo.
Schalke
Matarajio na uhalisia wakati mwingine huwa mambo tofauti sana kwa Schalke. Walimaliza nafasi ya 10 msimu uliopita- nafasi mbaya zaidi tangu miaka ya 90. Kocha Markus Weinzierl alifutwa kazi. Domenico Tedesco aliyechukua nafasi yake sasa ni kocha wa 5 ndani ya misimu mitatu. Je ataweza? Utabiri wa DW: Watafika katika Ligi ya Uropa.
Bayer Leverkusen
Bayer Leverkusen kufanya mambo tofauti msimu huu wa jua. Roger Schmidt yuko Beijing, Sven Bender aliungana na ndugu yake Lars huku Heiko Herrlich akisajiliwa na kocha kwa ghafla. Baada ya kunusurika kushushwa daraja msimu uliopita, lengo lao sasa ni kushiriki soka la Ulaya. Utabiri wa DW: Watamaliza katika nafasi za katikati ya jedwali.
FC Augsburg
Picha hii hapa juu inayo maana gani? Je Augsburg itakuwa katika nafasi ya mwisho ifikapo mwezi Mei? Kutokana na kwamba timu mbili mpya zenye uwezo mkubwa (Stuttgart na Hannover) zimepanda daraja - ni vigumu kwa Augsburg kunusurika. Timu hii ya Manuel Baum itahitaji kufanya kila iwezalo katika kila mechi. Utabiri wa DW: Augsburg itajikuta ikipambana isishushwe.
Hamburger SV
Hamburg ndiyo klabu pekee ambayo haijawahi kushushwa daraja tangu ligi ya Bundesliga ilipoanzishwa mnamo 1963. Lakini miaka minne iliyopita imekuwa ngumu kwao. Imekuwa na uchezaji usioridhisha mara mbili lakini ikanusurika. Je mwaka huu? Kocha Markus Gisdol na mkurugenzi wa michezo Jens Todt ni washawishi watulivu. Utabiri wa DW: Hamburg watakuwa salama.
1. FSV Mainz 05
Baada ya kushushwa daraja msimu uliopita, msimu huu unapaswa kuwa mwanzo mpya kwao. Ili kuendana na kaulimbiu yao ya 'Mwanzo Mpya', rais wa klabu amemuajiri kocha mpya Sandro Schwarz na mlinda lango mpya Rene Adler. Utabiri wa DW: Watakumbwa na matatizo ya kawaida ya kimfumo yanayozikumba timu zinazoelekea kushuka daraja.
VfB Stuttgart
Mabingwa hawa mara tatu wa Ujerumani wamerejea baada ya mwaka mmoja wakiwa katika ligi ya pili. Stuttgart imeimarisha kikosi chake chenye wachezaji wa umri mdogo pamoja na wawili wenye tajiriba wanaochezea timu ya taifa ambao ni mlinda lango, Ron-Robert Zieler, na mlinzi wa katikati, Holger Badstuber, kutoka Bayern Munich. Utabiri wa DW: Watamaliza katika nafasi ya katikati kwenye jedwali.
Hannover 96
Tangu kupandishwa daraja, Hannover haigongi tu vichwa vya habari kimichezo. Klabu yenyewe itapoteza udhibiti wake mwingi wakati Martin Kind atakapochukua uongozi. Mfumo wa 50+1 hautakuwepo tena. Hali hii imezua mgawanyiko huku mashabiki wakipiga vita klabu na Shirikisho la kandanda la Ujerumani. Utabiri wa DW: Itakumbwa na vurugu nyingi na kutishiwa kushushwa daraja.