1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande hasimu Libya zakutaka Moscow kujadili amani ya taifa

13 Januari 2020

Pande zinazohasimiana katika vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Libya zinakutana mjini Moscow kuidhinisha mpango wa kusitisha mapigano katika mazungumzo yanayoongozwa na maafisa wakuu wa Urusi na Uturuki.

https://p.dw.com/p/3W6dv
Libyen Tripolis Demonstration gegen die türkische Parlamentsentscheidung Truppen nach Libyen zu senden
Picha: Reuters/E. O. Al-Fetori

Mpango huo ambao ulikuwa uanze kufanya kazi siku ya Jumapili umeidhinishwa na Urusi na Uturuki kama njia moja ya kuyafufua mazungumzo ya amani katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika linalokumbwa na vita.

Kiongozi wa serikali inayotambuliwa Kimataifa Fayez al-Serraj, na mbabe wa kivita Khalifa Haftar, tayari wapo mjini Moscow Urusi, kuhudhuria mazungumzo ya leo Jumatatu yanayosimamiwa na wanadiplomasia wa ngazi ya juu na mawaziri wa ulinzi wa Urusi na Uturuki. Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Mevlut Cavusoglu na Waziri wa Ulinzi, Hulusi Akar ni miongoni mwa watakaohudhuria.

Mazungumzo haya yanakuja baada ya usitishwaji wa mapigano kupelekea kupungua kwa mapigano makali na mashambulizi ya angani siku ya Jumapili, licha ya kwamba pande zote mbili zinashutumiana kukiuka makubaliano hayo huku mapigano kadhaa yakishuhudiwa mjini Tripoli.

Fayez Serraj atoa wito kwa raia wa Libya kufugua ukursa mkpya wa amani Libya

Bildkombo Haftar und as-Sarradsch
Mbabe wa Kivita Libya Khalifa Haftar na Kiongozi wa serikali inayotambuliwa Kimataifa Fayez al-Serraj

Awali Sarraj aliwatolea mwito Walibya kufungua ukurasa mpya na kusonga mbele kueleke udhabiti na amani ya taifa hilo. Nae kiongozi wa baraza kuu la kitaifa la Libya Khaled al-Mechri amesema makubaliano ya leo ni njia moja muhimu ya kuelekea kupata suluhu ya kisiasa.

Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel wakati wa ziara yake mjini Moscow siku ya Jumamosi alisema Berlin ilitaka kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo kuendeleza juhudi alizoziita za kufana zinazofanywa na Urusi pamoja na Uturuki katika kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Libya.  

Hatua ya Urusi na Uturuki ya kujaribu kutafuta amani ya Libya inakuja miezi tisa baada ya mbabe wa kivita Khalifa Haftar kuanzisha mashambulizi mjini Tripoli. Uturuki inaiunga mkono serikali ya Libya ya Umoja wa Kitaifa GNA inayoongozwa na Fayez al-Serraj.

Libya, ambayo imekuwa katika mgogoro wa kisiasa tangu alipoondolewa madarakani na kuuwawa kiongozi wa muda mrefu nchini humo Muammar Gaddaffi ina serikali mbili hasimu tangu mwaka 2014. Mgogoro kati ya pande hizo mbili hasimu imelemaza uchumi wa taifa hilo, watu kulikimbia taifa hilo na kuusambaratisha mfumo wa usambazaji wa mafuta.

Chanzo: /dpa/ap/Reuters