1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Asia waukosoa utawala wa kijeshi Myanmar

11 Oktoba 2024

Viongozi wa mataifa 10 wanachama wa Jumuiya ya Kusini Mashariki Asia, wanaokutana kwenye mkutano wa kilele Laos, wamezikosoa juhudi za utawala wa kijeshi za utekelezaji wa mpango wa amani Myanmar, wakisema hazitoshi.

https://p.dw.com/p/4lfZW
ASEAN Gipfel
Picha: Sakchai Lalit/AP/picture alliance

Msimamo wa viongozi hao umechapishwa kwenye taarifa yao ya pamoja ambayo imeonekana na shirika la habari la AFP.

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewaambia viongozi kwenye mkutano huo leo Ijumaa kwamba Marekani ina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa shughuli za hatari zisizokubalika katika eneo la Bahari ya Kusini mwa China.

Blinken amewaahidi viongozi hao kwamba Marekani itaendelea kuunga mkono uhuru wa shughuli katika eneo hilo muhimu ambalo ni njia ya bahari ya shughuli za kibiashara.

Pembezoni mwa mkutano huo pia Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, amesema nchi hiyo inapaswa kuchukua hatua kutatua mvutano kuhusu suala la ushuru na Umoja wa Ulaya.

Michel ameonya kwamba mvutano huo unahatarisha kusababisha vita kamili vya kibiashara.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW