Viongozi wa Haiti wakubaliana kuunda serikali ya mpito
9 Aprili 2024Makubaliano hayo yanajumuisha baraza la wanachama tisa, lenye wapiga kura saba na waangalizi wawili, wanaowakilisha vyama vya siasa, sekta ya kibinafsi na mashirika ya kiraia, ambayo yatafungua njia kwa uchaguzi wa rais mapema 2026.
Jukumu la kwanza la baraza hilo ni kumchagua waziri mkuu ambaye, kwa ushirikiano na baraza hilo ataunda serikali yenye dhamana ya kuongoza nchi hadi "uchaguzi wa kidemokrasia, huru na wa kuaminika" utakapofanyika.
Zaidi ya watu 50,000 wakimbia mji mkuu wa Haiti
Aidha wajumbe wa baraza hilo au serikali itakayoundwa hivi karibuni hawatoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Kulingana na makubaliano hayo yaliyowasilishwa kwa Jumuiya ya Mataifa ya Karibia (CARICOM)mamlaka ya baraza hilo yatakamilika mnamo Februari 7, 2026.
Hata hivyo maelezo ya makubaliano hayo lazima yaidhinishwe na mamlaka inayoondoka madarakani.