1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waijadili DRC

1 Desemba 2024

Viongozi wakuu wa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki wamefanya juhudi kwa mara nyingine za kujaribu kuuleta amani mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/4ncFE
Tansania Arusha EAC-Gipfel
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania wakiwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika jijini Arusha.Picha: Philbert Rweyemamu/EAC

Viongozi hao waliokutana Jumamosi bado walishindwa kupiga hatua  kufuatia kutokuwepo kwa rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo na kuondoka mapema kwa mwenzake wa Rwanda katika mkutano huo wa kilele wa kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Taarifa iliyosomwa mwishoni mwa mkutano huo wa faragha mjini Arusha ilisema tu kwamba kuna haja ya kuzijumuisha pamoja juhudi zote za kutafuta amani ya kudumu Mashariki mwa Kongo. Rais Paul Kagame aliondoka muda mfupi baada ya mkutano huo lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kutoshiriki kwa Felix Tshisekedi. Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Salva Kiir wa Sudan,Samia Suluhu wa Tanzania,William Ruto wa Kenya,Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.