1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Viongozi wa Korea Kusini, China, Japan wakutana Soeul

27 Mei 2024

Viongozi wa Korea Kusini, China na Japan wanafanya mkutano wao wa kilele wa pande tatu mjini Seoul ambao ni wa kwanza katika karibu kipindi cha miaka mitano.

https://p.dw.com/p/4gJF3
Mkutano wa kilele kati ya Japan, Korea Kusini na China
Viongozi wa Korea Kusini, Japan na China wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka mitanoPicha: Lee Jin-man/AP/picture alliance

Kuna matarajio madogo ya mafanikio yoyote makubwa kwenye mkutano huo, lakini viongozi hao wameelezea matumaini huenda ukafufua diplomasia ya pande tatu na kutuliza mivutano ya kikanda.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeoul, Waziri Mkuu wa China Li Qiang, na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida watakutana leo kwa mazungumzo, huku tangazo la Pyongyang kuwa itarusha angani satelaiti kufikia Juni 4 likitarajiwa kuwa sehemu ya mada zitakazokuwa mezani. Korea Kaskazini iliwafahamisha walinzi wa pwani wa Japan kuhusu urushaji wa satelaiti hiyo katika kipindi cha siku nane kilichoanza usiku wa kuamkia leo.

Soma pia: Japan, Korea Kusini zatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Pyongyang imepigwa marufuku na maazimio ya Umoja wa Mataifa dhidi ya kufanya majaribio kwa kutumia teknolojia ya kurusha makombora. Baada ya mkutano huo wa kilele, Yoon, Li na Kishida watafanya kikao cha waandishi habari, kabla ya kujiunga na mkutano wa kilele wa biashara unaolenga kuimarisha biashara kati ya nchi hizo, ambao pia utahudhuriwa na viongozi wakuu wa kibiashara.