Viongozi wa NATO kufanya mazungumzo na Rais Zelensky
11 Julai 2024Matangazo
Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa NATO unaomalizika leo mjini Washington, Zelensky amewatolea wito washirika wa Ukraine hasa Marekani, kwenda mbali zaidi, ikiwemo kuvipa vikosi vyake vilivyozidiwa uwanja mpana zaidi wa kushambulia ndani ya Urusi.
Aidha, China imeionya NATO dhidi ya kuchochea mizozano katika uhusiano wake na Urusi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jin, ameitaka NATO kutoupeleka mzozo sawa na huo barani Asia.
Soma pia:NATO yashindwa kutoa mwaliko rasmi wa uanachama kwa Ukraine
Jana, viongozi wa NATO walitoa tamko la pamoja kuishutumu China kutokana na kuchukua jukumu muhimu la kuwa mwezeshaji mkuu wa Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.