1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa neo-Nazi kufikishwa mahakamani Jena.

21 Agosti 2023

Kesi dhidi ya watu 4 wanaotuhumiwa kuwa viongozi wa vuguvugu la harakati za siasa kali za kibaguzi nchini Ujerumani, ambalo linaendeleza mitizamo ya kinazi, imefunguliwa leo katika mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Jena.

https://p.dw.com/p/4VPt5
Protest against white supremacy and discrimination in Melbourne, Australia - 13 May 2023
Picha: Michael Currie/SPPA/ZUMA/picture alliance

 Jena, Ujerumani.

Watu hao wanatuhumiwa kuanzisha kile kinachojulikana kama kundi la ''Knockout 51''. Waendesha mashtaka wametuhumu kwamba washukiwa hao walikuwa wakipanga njama ya kuwauwa wanaharakati wa siasa za mrengo wa shoto na wawili kati yao wamedaiwa walikuwa wakimiliki silaha. Kwa mujibu wa waendesha mashataka wa shirikisho, Kundi hilo lenye makao yake katika mji wa Eisenach lilianza kupanga njama ya kuwauwa wanachama wa siasa kali za mrengo wa shoto Aprili mwaka 2021 au mapema zaidi. Kesi hiyo  imeendeshwa chini ya ulinzi mkali nje ya majengo ya mahakama.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW