1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visa vya COVID 19 vyazidi kuenea Uganda

Admin.WagnerD14 Juni 2021

Wasiwasi na taharuki vimetanda nchini Uganda wakati visa zaidi vya COVID-19 vikiendelea kuripotiwa kutoka sehemu mbalimbali za taifa hilo

https://p.dw.com/p/3urN5
Uganda Coronavirus Impfung
Picha: Luke Dray/Getty Images

Aidha familia kadhaa zimetumbikia katika majonzi kufuatia vifo vya watu wao waliougua ugonjwa huo wakakosa kupata matibabu stahiki kwa wakati.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya hadi watu 10,490 wamegunduliwa kuwa na virusi vya Corona katika kipindi cha wiki moja tu huku 15 wakifariki kwa siku moja tu mwishoni wa wiki siku mbili tu baada ya zuio la kutovuka mipaka ya wilaya lilipoanza kutekelezwa kwa muda wa siku 42.

Kasi hii ya maambukizi ieleta wasiwasi na mashaka wakati ambapo vituo vya afya vinaripoti kuzidiwa na wagonjwa wa COVID-19 huku vikipungukiwa na gesi ya oksijeni ambayo ni muhimu katika kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi. Jeshi laUganda limeingilia kati kuchangia katika kutengeneza gesi ya Oksijeni ili kukabiliana na uhaba wake katika vituo vya afya kote nchini.

Wakati huo huo, serikali imetoa wito kwa yeyote aliye na ujuzi wa kutengeneza gesi hiyo avisaidie vituo vya afya ili kuokoa maisha. Baadhi ya watu wana mtazamo kuwa kasi ya maambukizi inayoshuhudiwa kwa sasa imeongezeka kutokana na kupuuzwa kwa kanuni zilizowekwa.

Tiba asilia zatumika, wataalamu waonya

Kutokana na hofu na mashaka katika kutibu COVID-19, familia kadhaa zimegeukia dawa za miti shamba pamoja na malimao, tangawizi na pilipili kujitibu au kujikinga. Lakini wataalamu wa afya wanaonya dhidi ya matumizi haya.

Hata hivyo wataalamu wameonya dhidi ya mienendo ya watu kutumia mvuke katika jaribio la kujenga kinga dhidi ya COVID-19 hasa kwa watoto kwani mvuke huo unaweza kuchoma sehemu nyingine za mwili.