Vita Mashariki mwa DRC vyaendelea kusababisha umwagaji damu
21 Januari 2025Hayo yameelezwa na shirika la msalaba mwekundu na vyanzo vya wakaazi wa maeneo hayo. Mapigano yameongezeka katika wiki za hivi karibuni kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23, kundi linaloungwa mkono na Rwanda.
Mapigano hayo yalifika hadi kwenye milima ya Sake katika mji ambao uko kilomita kiasi 20 kutoka Magharibi mwa Goma.Waandishi wa habari wa AFP, waliripoti kwamba, kishindo cha miripuko kilisikika hadi Goma majira ya asubuhi hapo jana.
Wahusika wa vita DRC wamekiuka sheria ya kimataifa ya vita: Amnesty International
Taarifa pia zinasema Msikiti mmoja na makao makuu ya jeshi yamekimbiwa kkaribu na mpaka kati ya Kongo na Uganda.
Kukimbiwa kwa maeneo hayo kunaonesha uwepo wa harakati za waasi wenye silaha wa kundi la ADF linalotokea Uganda na ambalo limevamia eneo la Mashariki mwa Kongo kwa miaka na kusababisha umwagaji damu.