1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Vita vya Ukraine vyatimiza siku 500

8 Julai 2023

Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine leo amekitembela kisiwa kidogo cha Bahari Nyeusi kinachotajwa kuwa alama ya upinzani wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi ambao umetimiza siku 500 hii leo.

https://p.dw.com/p/4TcOj
Ukraine Wolodymyr Selenskyj
Picha: Ukrinform/ABACA/IMAGO

Zelensky ametumia ziara yake kwenye kisiwa cha Snake kutoa shukrani kwa wanajeshi wote wanaopambana kuilinda nchi hiyo.

Urusi ilikikamata kisiwa hicho katika saa za mwanzo za uvamizi wake nchini Ukraine, lakini walinzi wa kisiwa cha Snake walipata umaarufu ndani ya Ukraine na wale wanaoiunga mkono nchi hiyo baada ya kukataa kusalimu amri mbele ya meli ya kijeshi ya Urusi.

Walinzi hao walizidiwa nguvu na kuchukuliwa mateka na Urusi lakini baadae waliachiwa chini ya makubaliano ya kubadilishana mateka wa vita.

Kupitia ujumbe aloutoa kisiwani hapo, Zelenksy amesema Ukraine kamwe "haitadhibitiwa na wavamizi" kama ilivyokuwa kwa kisiwa cha Snake ambacho kilikombolewa na wanajeshi wa Ukraine mwezi Juni mwaka jana.